Mama mmoja akiwa na familia ya watoto wadogo watatu aliyejitambulisha kwa jina la Leticia Patrick anaomba msaada wa mtaji wa mama lishe kwa wasamaria wema ili aweze kulea watoto wake ikiwemo kuwalipia karo za shule,baada ya kukimbiwa kusikojulikana na mume na kumtelekeza bila hata sehemu ya kulala.
Kwa sasa mama huyu na watoto wake wanahifadhiwa na msamaria mwema katika maeneo ya Kiwalani,kwa binti Mussa tangu februari 22,mwaka huu ambapo mume wake aliyemtaja kwa majina ya Elias Samwel kwa maelezo ya mama huyo amedai kukimbilia Arusha.
LETICIA PATRICK - Mama aliyetelekezwa. |
Watoto wa mama aliyetelekezwa |
KUTOA NI MOYO WALA SIUTAJIRI
0 comments:
Post a Comment