Jamii imeaswa kuwashilikisha kina mama katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo ili kuweza kumnyenyua mwanamke kimaisha na kujenga taifa lenye usawa.
Akizindua ripoti ya mwaka mmoja ya mradi wa maji ya usafi wa vyoo mashuleni jijini Dar es salaam kwa niaba ya waziri wa maji injinia Mary Mbowe amesema kuna uhitaji mkubwa wa maji nchini hasa kwa kina mama vijiji ambapo serikali inaendelea kufanya juhudi mbalimbali za kutatua suala la maji ili kuweza kupunguza kero ya maji mjini na vijijini.
Aidha injinia Mbowe ameiambia jamii kuendelea kuwashirikisha kina mama katika miradi mbalimbali ya maendeleo hususani mradi ya maji vijijini na mijini ili kuleta mafanikio katika suala la maji.
MKURUGENZI MSAIDIZI WA WIZARA YA MAJI TANZANIA INJINIA - MARY MBOWE |
Mradi huo wa maji wa usafi wa vyoo mashuleni umefadhiliwa na serikali ya Austaria kupiti shirika lake la misaada.
0 comments:
Post a Comment