Image
Image

EXCLUSIVE: USIMAMIZI WA HUDUMA ZA BIMA YA AFYA, WATAKIWA KUWEPO NA CHOMBO KIMOJA.

Imeelezwa kumba upoulazima wa nchi kuwa na mfumo unaofanana na chombo kimoja ambacho kitasimamia huduma za bima ya afya unaotolewa na mashirika au makampuni mbalimbali nchini ili kuwawezesha watanzania kupata huduma bora kwa gharama inayostahili.

Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa mfuko wa taifa wa bima ya afya Balozi Ali Mchumo wakati anafungua mkutano wa baraza kuu la wafanyakazi wa mfuko huo, ambapo amesema kunahaja ya nchi kuwa na chombo kimoja kitakachosimamia uendeshaji wa bima ya afya ili kuwezesha huduma inayotolewa kuwa na ubora unaotakiwa na hata thamani ya fedha inayochangiwa na mwanachama ilingane na huduma anayopata.

Aidha Balozi Mchumo amesema changamoto inayoikabili NHIF ni kuendelea kutoa elimu ya umuhimu wa wananchi kujiunga na mfuko wa taifa wa bima ya afya ili waweze kuwa na uhakika wa afya zao.

BALOZI ALI MCHUMO- MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI- NHIF.
Balozi mchumo pia amesema malengo ya serikali ni ifikapo mwaka 2015 asilimia 30 ya watanzania wawe wamefikiwa na huduma ya bima ya afya na mwaka 2025 watanzania asilimia 75 wawe wamefikiwa na huduma hiyo,malengo aliyosema watayafikia iwapo changamoto ya uhaba wa dawa kwenye maeneo ya kutolea huduma pamoja na lugha mbovu kwa wateja yatarekebishwa.

Kwa upande wake mwenyekiti wa TUGHE tawi la bima ya afya Baraka Maduhu amesema changamoto inayowakabili wafanyakazi wa mfuko huo ni kuona namna gani wanaboresha huduma za wanachama wao pamoja na kuongeza idadi ya wanachama ili watanzania wengi waweze kunufaika na huduma za mfuko huo.

Mfuko wa taifa wa bima ya afya ambao umesambaa nchi nzima bara na visiwani, hivi sasa upo katika kampeni ya kuwaelimisha watanzania ambao sio waajiriwa waweze kujiunga na mfuko huo na ule wa afya ya jamii CHF ili ifikapo 2025 lengo la kuwafikia watanzania asilimia 75 liweze kufikiwa.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment