Image
Image

WAZIRI MKUU PINDA ATEMBELEA MAENEO YALIYOATHIRIWA NA GHASIA ZILIZOTOKEA MTWARA HIVI KARIBUNI.



Awali Waziri mkuu Mizengo Pinda alitembelea baadhi ya maeneo yaliyoathirika na matukio ya ghasia zinazodaiwa kuhusishwa na suala la gesi mkoani Mtwara wiki iliyopita.

Katika ziara yake hiyo aliyofuatana na Mkuu wa wilaya ya Mtwara Mikindani,Wilman Ndile, Mbunge wa Wilaya ya Mtwara mjini, Hasni Murji na kamati ya Ulinzi na usalama ya mkoa huo,Waziri mkuu ametembelea na kushuhudia uharibifu katika eneo la  sabasaba ndani ya uzio wenye ofisi nyingi ikiwemo taasisi ya uhasibu TIA,na kujionea namna ofisi ya ccm Chikongola ilivyochomwa moto.

Aidha,amejionea namna mahakama ya mwanzo ya Mikindani ilivyoharibiwa kufuatia ghasia hizo ambapo imefahamishwa kwamba nyaraka nyingi zenye mahusiano na mashauri yaliyoko mahakamani zilichomwa. 
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akipewa maelezo na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Wilman Ndile (kushoto) alipokwenda kuangalia jengo la Mahakama ya Mwanzo Mitengo mjini Mtwara jana.
 Amefika pia katika ofisi ya mbunge,Hasni Murji iliyochomwa pia ambapo nyuma yake ilichomwa baa ya mjasiriamali  mmoja na ofisi ya ccm kata Mtonya Mikindani na kusababisha hasara ya shilingi milioni 32.

Ameshuhudia pia nyumba ya waziri wa TAMISEMI Ofisi ya Waziri Mkuu,Hawa Ghasia iliyochomwa katika ghasia za mwezi Januari.

Kwa mjibu wa maelezo aliyopewa waziri mkuu,uchomaji katika eneo hilo,ulifanyika kuanzia majira ya saa nane mchana na vijana wenye umri wa miaka kati ya 16 na 25 huku wakiwa wameficha nyuso zao.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment