Taifa la Ethiopia
linapoteza karibu asilimia 16.5 ya pato lake la kitaifa kutokana na athari za
muda zinazotokana na utapiamlo miongoni mwa watoto kwa mujibu wa Shirika la
mpango wa chakula duniani WFP.
Hii ni moja ya takwimu
zinazoibuka kutokana na utafiti wenye kichwa "Gharama ya Njaaa barani
Afrika" kuonyesha athari za utapiamlo kwenye mataifa 12 tofauti, huku
taifa la Ethiopia likiwa la tatu matokeo yake kuchapishwa.
Kwa kipindi cha miaka
kumi iliyopita Ethiopia imepiga hatua muhimu katika kupunguza njaa na
utapiamlo.
Huduma za kutoa lishe zinazolenga akina mama na watoto na miradi
mingine ya kuboresha kilimo vimeziacha familia nyingi na afya bora na katika
hali nzuri ya kujilisha.
Hata hivyo, Shirika la WFP linasema
kuwa athari zinazotokana na utapiamlo ni gharama kubwa kwa uchumi wa Ethiopia.
Ripoti hiyo inakadiria kuwa utapiamlo unaigharimu Ethiopia mabilioni ya dola
kila mwaka.
0 comments:
Post a Comment