Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri
ya Kiislamu ya Iran leo amezindua Kiwanda cha Kusafisha Mafuta cha Lavan katika
kisiwa cha Ghuba ya Uajemi cha Lavan.
Kufuatia uzinduzi huo, uwezo wa Iran
wa kusafisha mafuta ya petroli kwa kiwango cha Euro-4 katika kiwanda hicho ni
mapipa milioni 2,800,000.
Kiwanda hicho kilichoko kusini mwa Iran pia kina
uwezo wa kuzalisha lita milioni moja za mafuta ya ndege kwa siku.
Akizungumza
katika uzinduzi huo, Rais Ahmadinejad amesema mradi huo ni muhimu sana kwa
kuzingatia kuwa maadui waliiwekea Iran vikwazo hasa vya petroli iliyosafishwa
ili kuzuia ustawi wa nchi hii.
Ameongeza kuwa, sekta ya mafuta Iran ilikuwa
tegemezi kwa usaidizi wa kigeni lakini nchi hii imeweza kujitegemea kikamilifu
baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Kwa muda mrefu pamoja na kuwa Iran ni mzalishaji mkubwa wa mafuta ghafi
ya petroli lakini ilikuwa ikinunua kutoka nje ya nchi petroli iliyosafishwa.
Hata
hivyo kufuatia mashinikizo ya Marekani baadhi ya mashirika yaliacha kuiuzia
Iran mafuta hayo.
Njama hizo za Marekani zimefeli baada ya Iran kufanikiwa
kujitosheleza kikamilifu katika usafishaji wa mafuta ya petroli.
0 comments:
Post a Comment