Nyota njema imeendelea kung'aa kwa kiungo wa kimataifa
wa Tanzania na klabu ya Simba ya Dar es Salaam, Shomary Kapombe, kufuatia
taarifa ya kutakiwa na klabu FC Twente inayoshiriki Ligi Kuu ya Uholanzi kwa ajili ya msimu ujao,kama atafanikiwa katika majaribio yake.
Kapombe ambye amekuwa katika kiwango bora cha soka
ameandika katika tovouti ya klabu hiyo ikieleza kwamba imekuwa ikimfutilia kwa karibu na kuridhiswa na kiwango chake cha soka anachokionyesha
akiwa na timu ya Tiafa Taifa Stars , pamoja na klabu yake ya Simba.
Taarifa kutoka klabu yake ya Simba imekaririwa ikisema
kwamba Kapombe mwenyewe ameonyesha nia thabiti ya kucheza Ulaya na amekuwa
akikataa ushawishi wa timu zingine za Tanzania zinazotaka kumng"oa ndani ya
Simba.
FC Twente inashiriki Ligi Kuu ya Uholanzi,
ilianzishwa mwaka 1926 na imekuwa katika
kiwango kizuri katika Ligi ya nchi hiyo ikiwapo kutwaa Kombe la KNVB na Johan Cruijff Schaal kwa
mwaka 2011, na wamekuwa mabingwa wa Ligi
Kuu kwa msimu wa 2009ñ2010,walikuwa pia washindi wa pili wa Kombe la
UEFA msimu wa 1974ñ1975.
0 comments:
Post a Comment