Rais wa Shirikisho la soka
nchini (TFF) Leodgar Tenga amewataka watanzania kuendelea kuinga mkono timu ya
soka ya Taifa a (Taifa Stars) ili iweze kufuzu kwenye fainali za Michuano ya
Afrika kwa wachezaji wa Ligi za Nyumbani
(CHAN) zinazotarajia kufanyika mwakani nchini Afrika Kusini.
Amesema kwamba Stars ambayo
ni timu changa imeonyesha maendeleo makubwa na kwamba itatumia uzoefu wa michuano ya kuwania kufuzu kombe la dunia ili kuweza
kufanya vizuri zaidi kwenye michuano hiyo ya CHAN hivyo ni wajibu wa kila
mtanzania kuwaunga mkono kwa nguvu zote.
Hata hivyo amesifia kiwango cha
soka barani afrika kuwa kimeanza kukua kulinganisha na siku za nyuma na kwamba
hali hiyo imechangia na mwamko ulijitokeza kwenye michuano mbalimbali zikiwemo
fainali hizo za kombe la CHAN.
Stars ambayo imeondolewa
kwenye michuano ya kuwani kufuzu kombe la dunia mwakani inatarajia kumenyana na
timu ya taifa Uganda The Cranes julai 13 mwaka huu kabla ya kurudiana wiki
mbili zijazo mjini Kampala.
Aidha Kuhusu Makocha,amewataka
kutumia ujuzi wao katika kuibua vipaji na kuendeleza sekta ya michezo nchini
huku baadhi ya wahitimu wa mafunzo hayo ya ukocha wakisema kwamba imewasaidia
katika maisha yao kama wanamichezo.
0 comments:
Post a Comment