Ripoti mpya kuhusu
mipango ya kimataifa ya kupunguza na kumaliza maambukizi mapya ya virusi vya
ukimwi miongoni mwa watoto ifikapo mwaka 2015 na kuwaongozea maisha mama zao
imeonyesha hatua zilizopigwa katika kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi
miongoni mwa watoto barani Afrika .
Ripoti hiyo inaonyesha kuwa nchi
saba zilizo kusini mwa jangwa la Sahara zikiwemo Botswana , Ethiopia, Ghana,
Malawi na Afrika Kusini zimepunguza maambukizi mapya ya virusi
vya ukimwi miongoni mwa watoto kwa asilimia 50 tangu mwaka 2009 huku mataifa
mengine mawili Tanzania na zambia nayo yakipiga hatua.
Ripoti hiyo
inaonyesha kuwa kulikuwa na visa 130,000 vya maambukizi ya virusi vya ukimwi
miongoni mwa watoto kwenye nchi hizo vikipungua kwa asilimia 38 tangu mwaka
2009.
Mkurugenzi mkuu wa Shirika la kupambana na ukinjwa wa ukimwi la Umoja wa
Mataifa UNAIDS Michel Sidibe anasema kuwa hatua zilizopigwa kwenye nchi nyingi
ni ishara tosha kuwa iwapo masuala muhimu yatazingatiwa watoto wanaweza
kuzaliwa bila ya virusi vya ukimwi.
0 comments:
Post a Comment