Uzalishaji na usambaziji wa maji katika jiji la dsm na
vitongoji vyake unatarajiwa kuongezeka kutoka lita milioni 300 hadi lita
milioni 756 kwa siku kiwango ambacho ni
mara mbili ya kinachozalishwa na kusambazwa sasa, ongezeko ambalo litatokana na
kukalimika kwa mradi mkubwa wa kusambaza maji kutoka Ruvu hadi jijini dsm.
Mshauri mhandisi wa mradi wa ujenzi wa mabomba, Rogers Mafuru amesema mradi huo unatarajiwa
kukamilika mwezi Machi mwakani ambapo baada ya kukamilika unatarijiwa kuzalisha
na kusambaza lita milioni 270 kwa siku ambapo pia bomba la zamani litaendelea
kutoa lita 180 milioni kwa siku
Nelly Msuya - Meneja Uhusiano - DAWASA |
John Moro - Diwani Kata ya Wazo. |
Kwa mujibu wa DAWASA baada ya kukamilika kwa mradi huo
upatikanaji wa maji katika jiji la dar es salaam utakuwa ni saa 24 tofauti na
ilivyo sasa ambapo maji yanapatikana kwa saa nane tu.
0 comments:
Post a Comment