Na Mwandishi wetu Faraja Kihongole aliyeko jijini Tanga
Ikiwa leo ni siku ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupinga matumizi ya biashara za dawa za kulevya baadhi ya
watumiaji wa dawa za kulevya ambao wapo kwenye nyumba maalum ya mafunzo ya
kuwasaidia kuachana na matumizi ya dawa hizo, wameitaka jamii kutothubutu
kutumia dawa hizo kutokana na madharadhi yake.
Mateja hao wanaoishi kwenye kituo kijulikanacho kwa
jina la TANGA SOBER HOUSE, ambao wengine wameshatumia dawa hizo kwa zaidi ya
miaka thelathini na wengine alishawahi kufanya kazi serikalini wanasema kutumia
dawa za kulevya si ujanja na hakuna teja special, kwani madhara yatokanayo na
matumizi ya dawa za kulevya yanafanana kwa mateja wote na kwamba unapoanza
kutumia madawa hayo ni sawa na kusimamisha maisha yako kwa sababu unakuwa huna uwezo
tena wa kufikiria maendeleo ya maisha yako binafsi, familia, jamii na nchi kwa
ujumla.
Ujumbe kutoka umoja wa mataifa ofisi ya tanzania
umeendesha kongamano la vijana zaidi ya mia mbili mjini Tanga ikiwa ni sehemu
ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupinga matumizi na biashara haramu ya
madawa ya kulevya ambayo hufanyika tarehe 26 June kila mwaka, na kitaifa
maadhimisho hayo yamefanyika mjini Dodoma.
0 comments:
Post a Comment