Jeshi la polisi kanda maalum Dar es Salaam limepiga
marufuku maandamano yaliyoandaliwa na chama cha wananchi Cuf kwenda ikulu siku ya ijumaa wiki hii kwa
madai ya kumshinikiza Rais Jakaya Kikwete kulipangua jeshi la polisi pamoja na
kutafutia ufumbuzi mgogoro wa gesi ya mtwara.
Kamishna wa polisi kanda maalum dsm CP SULEIMAN KOVA amesema
maandamano hayo yamepigwa marufuku baada ya kupokea barua kutoka ikulu kuwa
rais Kikwete hatakuwa na nafasi ya kupokea maandamano hayo kutokana na ujio wa
marais watakaoshiriki mkutano wa Smart Partnaship Dialogue mwisho ni mwa wiki.
jeshi hilo pia limeonya wale wanaotakata kuaandaa
mabango na maandamano wakati wa ujio wa rais wa marekani Barack Obama kwamba
watachukuliwa hatua za kisheria, kufuatia taarifa za kuwepo kwa mpango huo.
Aidha katika kupambana na matukio ya uhalifu jeshi
hilo limewatia mbaroni watuhumiwa wa ujambazi ishirini na wawili kati yao ni
raia wa burundi wakiwa na silaha nne
aina ya SMG pamoja na bastola mbili zikiwa na risasi zaidi ya sitini. Hatua
hiyo imefikiwa baada ya kufanyika operesheni maalum ambapo katika mapambano ya
kurushiana risasi mmoja wa watuhumiwa alifariki dunia.
0 comments:
Post a Comment