Kituo cha sheria na haki za binadamu - LHRC kimesema kinaendesha mchakato wa kukusanya maoni kutoka kwa wadau mbalimbali na kisha kuandaa waraka kupinga kauli ya waziri Mkuu Mizengo Pinda bungeni ambayo kituo hicho kinadai imebariki vyombo vya ulinzi na usalama hususan jeshi la polisi kuwapiga wananchi watakaokaidi na kupinga amri halali ya jeshi hilo.
LHRC na baadhi ya wadau hao wanamtaka waziri mkuu
Mizengo Pinda kufuta kauli yake hiyo sambamba na kulielekeza jeshi la polisi
kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na
taratibu zilizoko katika kutekeleza majukumu yake ya kulinda usalama wa raia na mali zake.
Mizengo Pinda - waziri mkuu Tanzania |
Kauli hiyo imekuja muda mfupi wakati akizungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es
salaam, Ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC Dk Hellen Kijo Bisimba, amedai kuwa kwa
sasa maudhui ya kauli hiyo ni kinyume na cha katiba, sheria za nchi na misingi
ya haki za binadamu hasa katika kipindi hiki ambacho kumekuwa na matukio mengi
ya ukiukwaji wa haki za binadamu yanayodaiwa kuhusisha na vyombo vya dola.
0 comments:
Post a Comment