Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa
Afrika Kusini amesema kuwa, mafanikio ya uchaguzi mkuu ujao wa Zimbabwe, licha
ya kuinufaisha nchi hiyo bali utakuwa na taathira ya kiusalama katika eneo lote
la kusini mwa Afrika.
Ibrahim Ibrahim
amesema kuwa, uchaguzi wa Zimbabwe uliopangwa kufanyika Julai 31 mwaka huu
utapelekea kuboreka hali ya kiuchumi na kijami pamoja na kunyanyuliwa kiwango
cha maisha ya wananchi wa Zimbabwe.
Wananchi wa
Zimbabwe wapatao milioni sita waliotimiza masharti ya kupiga kura, siku ya
Jumatano ijayo wataelekea kwenye masanduku ya kupigia kura kwa shabaha ya
kumchagua rais pamoja na wabunge zaidi ya 200 na madiwani wapatao 2,000 nchini
humo.
Tume ya
Uchaguzi ya Zimbabwe imetangaza kuwa, mgombea wa kinyang’anyiro cha
urais atakayepata asilimia 51 ya kura za wananchi atatangazwa mshindi,
kinyume cha hivyo duru ya pili ya uchaguzi wa rais itafanyika mwezi Septemba.
Mchuano mkali wa
nafasi ya rais unashuhudiwa kati ya rais wa sasa Robert Mugabe kutoka Zanu PF
na Morgan Tsvangirai Waziri Mkuu na ambaye pia ni kiongozi wa chama cha MDC.
Imeelezwa kuwa, hadi sasa karibu waangalizi
600 wa kigeni wako nchini Zimbabwe kwa shabaha ya kusimamia uchaguzi huo.
0 comments:
Post a Comment