Chama cha 'Tiako I Madagasikara' kinachofungamana na
Marc Ravalomanana rais wa zamani wa Madagascar kwa mara nyingine tena kimepinga
mpango wa kundi la kimataifa la mawasiliano lililopewa jukumu la kuutatua
mgogoro wa Madagascar.
Chama hicho kimesisitiza kuwa vitisho vya kundi hilo
na jumuiya nyingine za kimataifa, havitaweza kubadilisha msimamo wa chama
hicho.
Mpango huo unawataka wagombea watatu wajiengue kwenye
kinyang'anyiro cha uchaguzi ujao wa rais nchini humo.
Kundi la kimataifa la mawasiliano liliwataka Andry
Rajoelina rais wa sasa wa serikali ya mpito ya Madagascar, Didier Ratsiraka
rais wa zamani wa nchi hiyo pamoja na Lalao Ravalomanana mke wa Marc
Ravalomanana rais wa zamani wa nchi hiyo wasishiriki kwenye uchaguzi ujao,
kwani ushiriki wao unakinzana na katiba ya nchi hiyo.
Baada ya kufanyika mapinduzi nchini Madagascar
yapata miaka mitano iliyopita, na kuundwa serikali ya mpito, nchi hiyo imekuwa
ikishuhudia migogoro ya kisiasa siku hadi siku.
0 comments:
Post a Comment