Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetoa mkono wa pole kwa
serikali na wananchi wa Uhispania kutokana na ajali ya treni iliyotokea hivi
karibuni nchini humo na kupelekea watu wasiopungua 80 kufariki dunia na wengine
wasiopungua 140 kujeruhiwa 20 na hali zao zikielezwa kuwa mahututi.
Sayyid Abbas Araqchi
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje wa Iran amesema kuwa, ajali hiyo ya
treni imeleta majonzi ulimwenguni kote, hivyo serikali pamoja na wananchi wa
Iran wanaungana na wenzao wa Uhispania kwenye kipindi hiki kigumu cha huzuni na
maombelezo.
Ajali hiyo ilitokea siku ya Jumatano, pale treni hiyo ilipo kuwa inatembea
mwendo wa kasi katika kona na kusababisha mabehewa 13 kuondoka kwenye
reli, na manne kupinduka kabisa.
Taarifa zinasema kuwa, dereva wa treni hiyo
anashikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi, ingawa alishatoa tahadhari ya
kuanguka kwa treni hiyo, baada ya kushindwa kuidhibiti treni hiyo iliyokuwa
kwenye mwendo wa kasi.
Treni hiyo ilikuwa ikitoka Madrid na
kuelekea El Ferrol, na kupata ajali katika mji wa Santiago de Compestela,
ulioko katika mkoa wa Galicia.
Hii inahesabiwa kuwa ajali mbaya zaidi ya treni
kutokea nchini humo tokea mwaka 1972.
0 comments:
Post a Comment