Mkurugenzi wa Tanesco, Felchesmi
Mramba (wa tatu kushoto) sambamba na mwakilishi wa shirika la kimataifa la JICA,
Yasunori Onishi.jijini Dar es Salaam.
Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (Jica)
limelikabidhi Shirika la Umeme Nchini (Tanesco), kituo cha kupozea umeme
kilichopo wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam baada ya kukifanyiwa ukarabati
uliogharimu Dola za Marekani 500,000.
Makabidhiano hayo yaliyokwenda sambamba na kutiliana
saini yalifanyika jijini Dar es Salaam
baina ya Kaimu Mkugenzi wa Tanesco, Felchesm Mramba na Mwakilishi wa Jica,
Yasonari Orishi ambaye aliongozana na ujumbe wa shirika hilo kutoka Japan.
Mramba alisema kukabidhiwa kwa kituo hicho ni hatua
nzuri kwani inaimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika katika jijini Dar
es Salaam na kwamba Jica wamefunga mitambo ya kisasa inayotumia gesi.
Ukarabati
wuliofanywa katika kituo hicho ni utekelezaji wa mipango ya uboreshaji wa
upatikanaji wa umeme na kwamba kuna vituo vingine vipya vinavyotarajia kujengwa
eneo la Kurasini, Mbagala, Gongolamboto na Kinyelezi.
Aliongeza kwa kusema kuwa vipo vituo vingine 18
vinavyojengwa na kukarabatiwa katika jiji la Dar es Salaam na kuwataka wakazi
wa jiji hilo kuwa wavumilivu kwani tatizo la upatikanaji wa umeme ufumbuzi wake
utapatikana hivi karibuni.
0 comments:
Post a Comment