Mshambuliaji wa AZ Alkmaar Jozy Altidore anatarajiwa kuwa na
mazungumzo na Sunderland baada ya vilabu hivyo viwili kukubaliana juu ya mpango
wa mauzo ya nyota huyo raia wa Marekani.
Mshambuliaji huyo
mwenye umri wa miaka 23 ambaye amewahi kuichezea Hull City katika ligi kuu ya
Englanda Premier League msimu wa 2009-10, anatarajiwa kuelekea England kwa
ajili ya vipimo vya afya jumatatu.
Altidore alipokuwa
na umri wa miaka 19 alijiunga na Hull City kwa mkopo wa muda mrefu akitokea
Villarreal mwezi August 2009.
Alifunga goli zuri
katika wa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Manchester City February 6 2010, likiwa
ni goli lake pekee alilowahi kufunga katika jumla ya michezo 28 ya michezo ya
ligi kuu ya England Premier League.
Alkmaar
imethibitisha kuwepo kwa makubaliano kupitia mtandao wa klabu hiyo lakini
imeshindwa kuweka wazi ni mpango wa kiasi gani cha fedha.
Altidore amesaliwa
na miaka ndani ya mkataba wake na klabu hiyo ya kidachi.
Sunderland
iliyochini ya Paolo Di Canio ikiwa itafanikiwa kumsajili Altidore,
itakuwa ni klabu ambayo ilikuwa bize kweli kweli katika zoezi la usajili kwani
tayari imekuwa katika mipango ya kusajili wengine saba.
Sunderland kwa jina
la utani Paka mweusi pia wamethibitisha kuwasajili akina Modibo Diakite,
Valentin Roberge, Cabral, Duncan Watmore, David Moberg Karlsson na mlinda
mlango Vito Mannone.


0 comments:
Post a Comment