Licha
ya kutopata nyota wake inaowasaka kuimarisha mashambulizi, Arsenal wamewakata maini Manchester
City kwa kuwatandika mabao 3-1.
City
wanaofundishwa na kocha mpya, Manuel Pellegrini, wanafikiriwa kuwa na washambuliaji wakali zaidi kwa msimu
unaoanza Jumamosi ijayo.
Arsenal
walionekana kupewa nguvu ya aina yake na Theo Walcott aliyecheza vyema katika mechi ya kirafiki
iliyopigwa nchini Finland.
Washika
Bunduki wa London walianza kucheka na nyavu katika dakika ya 24 kwa bao
lililofungwa na Walcott aliyemchambua kipa Joe Hart
kwa juu, baada ya kupasiwa vyema na Aaron Ramsey aliyemaliza msimu uliopita vyema.
Kwa
matokeo hayo, Arsenal wamemaliza programu yao ya kujiandaa kwa Ligi Kuu kwa
ushindi katika mechi tano, sare moja na kufungwa moja, tangu kuanza kwa ziara
hizo Julai.
City kwa upande wao wameshinda mechi
tatu na kufungwa nne, hitimisho likiwa hiyo ya Jumamosi hii jioni.
Walcott
alifunga tena bao la pili baada ya mapumziko, akitengewa pia na Ramsey, kisha
akampiga chenga kipa Hart kabla ya kutundika mpira kwenye kamba.
Alikuwa
walcott tena aliyesababisha kilio Etihad, lakini safari hii alimpigia pasi
mshambuliaji Mfaransa, Olivier Giroud
ambaye hakufanya ajizi kujaza mpira golini.
Mshambliaji
mpya wa City aliyetoka Sevilla ya Hispania, Alvaro Negredo alifunga bao la
kufutia machozi kwa kumzidi maarifa kipa Lukasz Fabianski kwa kupitisha mpira
pembeni mwake katika dakika ya 80.
Arsenal
wanaanza kipute chao kwa kuwakaribisha Aston Villa Emirates Jumamosi, wakati
City watakuwa wenyeji wa Newcastle hapo Etihad Jumatatu inayofuata.
Vikosi
vilivyochuana vilikuwa hivi – Arsenal: Szczesny (Fabianski 46); Sagna
(Jenkinson 73), Mertesacker, Koscielny, Gibbs; Arteta (Perez 67), Wilshere
(Cazorla 46), Ramsey (Hayden 88); Oxlade-Chamberlain (Zelalem 73), Walcott,
Podolski (Giroud 46).
Manchester
City: Hart; Zabaleta (Richards 46), Kompany, Lescott (Boyata 85), Clichy;
Milner (Jesus Navas 46),
Fernandinho (Rodwell 79), Toure (Javi Garcia 67), Silva (Jovetic 67); Dzeko
(Nasri 46), Negredo.
0 comments:
Post a Comment