RAIS JAKAYA KIKWETE AKISALIMIANA NA MEYA WA BUKOBA DK ANATORY AMANI HIVI KARIBUNI.
KAMATI
Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CC-CCM) kimeiomba Serikali kumtuma Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh kwenda Bukoba, Kagera
kuchunguza tuhuma dhidi ya Meya wa Manispaa hiyo, Dk Anatory Aman.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana mjini Dodoma, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM,
Nape Nnauye alisema kamati hiyo imewaagiza
Mbunge wa Bukoba Mjini, Khamis Kagasheki na Dk Aman kurudisha utulivu wa
kisiasa katika Manispaa hiyo ambayo katika siku za karibuni imekuwa na mgogoro
mkubwa.
Alisema
Kamati Kuu inaamini kuwa kwa CAG kwenda Bukoba kutasaidia kujulikana kwa mambo
anayolalamikiwa ili ukweli ujulikane na hatua stahiki zichukuliwe.
Alisema
CAG ametakiwa kwenda haraka Bukoba na uchunguzi unatakiwa kufanyika katika
kipindi cha muda mfupi kuanzia jana.
“Hivi
ninavyozungumza ama CAG ameondoka kuelekea Bukoba au yuko katika maandalizi ya
kwenda Bukoba kufanya uchunguzi huo na ukweli utajulikana.
Hatuna hofu juu ya
kwenda CAG maana katika kikao hiki yupo Waziri Mkuu na vyombo vingine kwa hiyo
wamewasiliana naye,” alisema Nape.
Nape
alisema wamelazimika kuitaka Serikali kumtuma CAG kwa kuwa tume iliyotangulia
iliyomhusisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,
Dk. Rehema Nchimbi haikuwa ya kiuchunguzi, bali ilishughulikia suala la
migogoro.
Alisema
kuwa taarifa ya uchunguzi huo inapaswa kupelekwa katika kikao cha Baraza la
Madiwani wa Manispaa ya Bukoba ili waijadili na kuchukua hatua stahiki kwa
mujibu wa kanuni za uendeshaji wa halmashauri hiyo.
Dk Aman
anapingwa kutokana na hatua yake ya kuanzisha miradi ya kupima viwanja vya Mji
wa Bukoba, ukarabati wa soko na ujenzi wa stendi kuu ya mabasi ambayo inadaiwa
kuwa na harufu ya ufisadi.
Madiwani
wapeta
Akizungumzia
kubatilishwa kwa uamuzi wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Mkoa wa Kagera wa
kuwafukuza uanachama madiwani wanane wa Manispaa ya Bukoba, Nape alisema uamuzi
huo ulikiuka Katiba ya CCM ya mwaka 1977 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2012.
Alitaja
kifungu kilichokiukwa kuwa ni Ibara ya 93 (15) ambacho kinataka CC kujulishwa
uamuzi huo kabla ya kuchukuliwa kwa hatua hiyo.
“Kamati Kuu inawataka madiwani wa CCM wa Manispaa
ya Bukoba, Mbunge wa Bukoba na Meya wa Manispaa hiyo kurudisha utulivu katika
halmashauri yao.
Pia kurudisha mshikamano katika chama ili Ilani ya CCM
itekelezwe kama ilivyokusudiwa,” alisema Nape.
MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment