Mansoor Yusuf Himid.
Halmashauri
Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) imeridhia uamuzi wa Halmashauri Kuu
ya chama hicho Wilaya Mjini Magharibi Zanzibar wa kumvua uanachama wa chama
hicho Mwakilishi wa Kiembe Samaki
Mansoor Yusuf Himid.
Akizungumza
na waandishi wa habari mara baada Halmashauri Kuu ya Taifa kumaliza kikao
chake, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa (CCM) Bw. Nape Nnauye amesema kikao hicho
kimeridhika na tuhuma zilizokuwa zinamkabili mjumbe huyo wa Baraza la
uwakilishi.
Aidha, Kwa
mujibu wa Katibu huyo mwenezi wa (CCM) kikao hicho cha Halmashauri Kuu ya
Taifa, kimewateua Bw. Romuli Rojas John, Bw. Kassim Mabrouk Mbarak na Bi. Mary
Maziku, kuwa makatibu wa mikoa, ambapo watapangiwa vituo vya kazi hapo baadaye.
Kuhusu,
sakata la madiwani wa (CCM) Bukoba Mjini, Bw. Nape amesema maamuzi yatatolewa
baada ya viongozi wote husika kusikilizwa na Kamati kuu ya Halmashauri kuu ya
Chama hicho.
0 comments:
Post a Comment