Mtandao wa Sky Sports umesema vyanzo vyake
vya kuaminika vya habari vimeuambia mtandao huo kwamba Tottenham wanafikiria
kukubali ofa kutoka kwa klabu kadhaa kwa ajili ya Gareth Bale - na kusisitiza
kwamba bado hawajakubaliana na Real Madrid kumuuza winga huyo.
Real wamekuwa wakiongoza mbio za
kumsajili Bale wakati wa dirisha hili la usajili, lakini sasa kumetokea klabu
nyingine ambayo inaipa upinzani katika kushinda mbio za kumsaini Bale.
Ripoti nchini Spain wikiendi hii
zilikuwa zikisema kwamba Madrid walikuwa wanamalizia taratibu za mwisho za
kumsaini Bale katika dili ambalo lingevunja rekodi ya dunia - huku Spurs
wakiripotiwa kukubali kumuuza nyota huyo.
Japokuwa, sasa imefahamika hakuna
makubaliano yaliyofikiwa baina ya Tottenham na Real na sasa klabu hiyo ya White
Hart Lane inafikiria ofa za klabu nyingine.
Manchester United wamekuwa wakitajwa kuvutiwa
na Bale, lakini inabaki kusubiriwa kama David Moyes ndio kocha mwingine
aliyejiingiza katika mbio za kumtaka winga huyo mwenye miaka 24.
0 comments:
Post a Comment