Sekretarieti
ya Baraza la Katiba la wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa
limependekeza uraia wa nchi mbili uwe haki ya kikatiba kama zilivyohaki
nyingine huku ikitaka muungano wa serikali mbili uendelee na mapungufu
yafanyiwe marekebisho.
Aidha Baraza
hilo limependekeza kuwa katika sera ya mambo ya nje ambayo inajumuisha uteuzi
wa mabalozi, Rais baada ya kuteua mabalozi bunge kupitia kamati
inayoshughulikia mambo ya nje uteuzi huo uidhinishwe na taasisi hiyo ya umma.
Akiongea na
wanahabari mara baada ya ufunguzi wa kikao cha baraza hilo la mchakato wa
katiba mpya,mwenyekiti wa baraza hilo,Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa
kimataifa BERNARD MEMBE ametoa rai kwa asasi, taasisi na makundi ya watu
walioruhusiwa na tume ya mabadiliko ya katiba kisheria watumie fursa hiyo
kukusanya maoni kwa jamii badala ya kufanya mikutano ya hadhara.
Baraza hilo
lililowajumuisha watumishi mbalimbali waandamizi wa wizara hiyowakiwemo
wastaafu katika ngazi ya uwaziri na mabalozi wa Tanzania katika nchi mbalimbali
ambapo mjumbe wa Tume ya mabadiliko ya katiba,Dk,SALIM AHMED SALIM
ameyasisitiza mabaraza kusaidia marekebisho yaliyomo katika rasimu ya katiba
mpya ili kutengeneza katiba ya wananchi na sio ya kikundi fulani.
0 comments:
Post a Comment