Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Ludovic Utouh amesisitiza umuhimu wa
ushirikishwaji wa umma katika mchakato wa ukaguzi mbalimbali unaohusu
rasilimali za umma ili kuongeza uwazi na uwajibikaji katika matumizi na
udhibiti wa rasilimali za taifa hususan fedha za umma.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam katika semina kwa watendaji mbalimbali wakiwemo wabunge,
watendaji wa halmashauri, wakaguzi wa ndani na nje ya nchi pamoja na
wawakilishi wa asasi za kiraia,Bwana Uttoh, amesema suala la uwazi na
uwajibikaji katika ngazi ya jamii halipaswi kuachwa kwa taasisi za ukaguzi
pekee, bali linapaswa kushirikisha jamii kupitia asasi zisizo za kiserikali
pamoja na vyombo vya habari.
Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu huyo wa hesabu za serikali amesema semina hiyo ya siku mbili
iliyoandaliwa na ofisi ya taifa ya ukaguzi (NAOT), imelenga kujenga uwezo wa
namna ambavyo wanaweza kushirikisha umma katika ukaguzi na kufikia katika
mapendekezo ya namna wananchi ambao ndio wahusika wakuu watashirikishwa katika
zoezi hilo muhimu na kupata njia tofauti za kushirikisha umma.
Nao washiriki
wa semina hiyo wamesema ushirikishwaji uliokuwepo ni wananchi kupatiwa taarifa
kwa kubandikiwa katika mbao za matangazo kwenye halmashauri za wilaya, hali
ambayo haikuwa ya ushirikishwaji kikamilifu na kwamba wanamatumaini semina hiyo
itasaidia kubaini njia muafaka za ushirikishwaji wa umma.
Wakaguzi
kutoka nje ya nchi wanaoshiriki semina hiyo ni pamoja na kutoka Ufilipino,
India pamoja na Argentina.
0 comments:
Post a Comment