Jumuiya ya
Ulaya imekabidhi kiasi cha Shilingi Bilioni 101 kwa Serikali ya Tanzania, ikiwa
ni msaada wa Kibajeti kwa ajili ya kuimarisha zaidi maeneo muhimu kwenye
malengo ya Millenia MDG.
Akizungumza
katika hafla ya makabidhiano jijini Dar es salaam, Waziri wa Fedha, Dk.William
Mgimwa amesema fedha hizo zinalenga kuiongezea uwezo Serikali ya Tanzania
katika kupunguza umasikini, ili kufikia malengo ya Maendeleo ya Millenia.
Mwaka 2009
Serikali ya Tanzania ilisaini makubaliano na Jumuiya ya Ulaya ambapo EU itatoa
Euro Milioni 305 ambazo ni sawa na shilingi Bilioni 654.7 kwa serikali ya
Tanzania ili kuiwezesha kutekeleza maeneo muhimu kwenye Malengo ya Maendeleo ya
Millenia kwa kipindi cha miaka sita.
Kwa upande
wake, Balozi wa Jumuiya ya Ulaya hapa nchini Filberto Sebregondi amesema Umoja
wa Ulaya umeridhika na hatua chanya zinazochukuliwa na Tanzania kuelekea
malengo ya Maendeleo ya Millenia.
Misaada ya
Jumuiya ya Ulaya na washirika wengine wa kimaendeleo, imeisaidia kwa kiasi
kikubwa serikali ya Tanzania kupambana na umasikini.
0 comments:
Post a Comment