Image
Image

WANAJESHI 146 WA JWTZ WATUNUKIWA NISHANI


                    Jenerali Davis Mwamunyange.
 Mkuu wa Jeshi la Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania (JWTZ)Jenerali Davis Mwamunyange kwa niaba ya Amiri Jeshi wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Rais Jakaya Mrisho Kikwete ametunuku nishani mbalimbali maafisa na askari wa jeshi hilo wapatao 146 baada ya kutumikia jeshi hilo kwa muda mrefu.

Katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye viwanja vya wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga Taifa, jijini Dar es Salaam askari wapatao 51 watunikiwa nishani ya utumishi wa muda mrefu na tabia njema, askari sitini na watatu nishani ya utumishi wa muda mrefu, maafisa ishirini na watatu nishani ya utumishi uliotukuka na askari 10 nishani ya ushupavu.

Kwa upande wao askari waliovishwa nishani hizo wamewataka wananchi kujitoa bila ya woga katika kuwafichua watu wanaoshiriki vitendo viovu dhidi ya jamii na taifa kwa ujumla 




Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment