Jeshi la
polisi kanda maalum limetoa ufafanuzi kuhusu kifaa kilichodhaniwa kuwa ni Bomu
kilichoonekana katika eneo la kanisa la kkkt usharika wa kijitonyama jijini dsm
jana ambapo limesema baada ya uchunguzi imegundulika kuwa ni kifaa cha kunasia
sauti anga za juu kinachotumiwa na mamlaka ya hali ya hewa.
Akizungumza
na waandishi wa habari huku akiwa na mataalamu kutoka mamlaka ya hali ya hewa
Kamanda wa kanda maalum Kamishna wa Polisi Suleiman Kova amesema kifaa hicho
kinachojulikana kama radio sonde huwa kinarushwa kila siku huku kikiwa
kimefungwa puto (baloon) na baada ya kuruka umbali wa kilometa elfu ishirini
balooni hupasuka na kifaa hicho kurudi ardhini .
Akizungumzia
matukio ya uhalifu kamanda Kova amesema jumla ya watuhumiwa 136 wamekamatwa
kati yao majambazi hatari wanne wakiwa na bastola mbili pamoja na risasi
36,ambapo pia jeshi hilo linaendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio la bomu la
kienyeji lililorushwa katika kanisa la kkkt tabata pamoja uchunguzi dhidi ya
watumishi bandia wa vyombo vya dola waliokamatwa hivi karibuni.
Wakati huo huo kampuni ya simu ya mkononi ya vodacom imaenzisha utaratibu maalum wa m-pesa utakaotumiwa na makampuni makubwa ili kulipa mishahara kuepuka vitendo vya uporaji wakati wa kusafirisha fedha.
0 comments:
Post a Comment