Mwalimu wa Shule ya Msingi
Morotonga, wilayani Serengeti, Mkoa wa Mara, Karata Mugunda, anashikiliwa na
Jeshi la Polisi wilayani hapa, kwa tuhuma za kumpiga na kumlisha kinyesi mtoto
wake wa kumzaa mwenye umri wa miaka 10.
Mwenyekiti Mtendaji wa Kituo cha
Sheria na Haki za Binadamu, Wilaya ya Serengeti, Samwel Mewama, alithibitisha
kutokea kwa tukio hilo na kwamba mtoto huyo alilish
wa kinyesi alichokuwa amejisaidia
ndani ya nyumba yao.
Kwa mujibu wa Mewana, tukio hilo
la kusikitisha lilitokea Agosti 14, mwaka huu saa 12 alfajiri.
“Chanzo cha tukio hili la
kikatili ni mtoto huyo kujisaidia haja kubwa ndani ya nyumba, baada ya kuogopa
kutoka nje usiku wa manane.
“Baada ya kujisaidia, baba yake
ambaye ni mwalimu, alikasirika na kuamua kumwadhibu kwa kumchapa fimbo sehemu
za makalio na kumsababishia majeraha ya kutisha.
Pamoja na kumwadhibu kwa fimbo,
alimlazimisha ale kinyesi chote alichojisaidia kisha akamlazimisha anywe maji
kwa wingi,” alisema Mewana.
Akizungumzia jinsi alivyopata
taarifa za tukio hilo, alisema ofisi yake ilipigiwa simu na mwalimu mmoja
anayefundisha shule moja na mtuhumiwa.
Baada ya taarifa hiyo,
alifuatilia ili kujua ukweli wake ndipo alipomkuta mwanafunzi huyo akiwa
amejeruhiwa vibaya makalio yake.
“Kwa kweli nilimkuta ana hali mbaya,
kwa hiyo nilichokifanya nilimchukua na kumpeleka Kituo cha Polisi Mugumu
nikapewa PF 3 kwa ajili ya matibabu hospitalini,” alisema.
Aliongeza kwamba, baada ya polisi
kupata taarifa hiyo na kushuhudia majeraha aliyokuwa nayo mwanafunzi huyo
kupitia dawati lao la kijinsia, walikwenda kumkamata mwalimu huyo ili hatua
zaidi ziweze kufuata.
Daktari wa Zamu katika Hospitali
ya Nyerere DDH, Dk. Ohoka Joseph, alithibitisha kuwapo kwa tukio hilo.
Alisema mtoto huyo alijeruhiwa
vibaya kwenye makalio yake na kwamba ameathirika kisaikolojia.
Mwenda pole na upole wake blog.


0 comments:
Post a Comment