Rais Jakaya Kikwete, amevitaka Vyuo Vikuu na
vyuo Vishiriki nchini kuongeza udahili wa wanafunzi, pamoja na kutoa shahada za
uzamili na uzamivu kwa wingi ili kuongeza wakufunzi wengi watakaosaidia kuinua
kiwango cha elimu nchini.
Kadhalika Rais Kikwete ameiagiza Wizara ya Elimu
na Mafunzo ya Ufundi, kuhakikisha wanatekeleza mpango wa kukuza elimu wa
‘matokeo makubwa sasa’ ili kuondokana na changamoto zinazozikabili nchi kwa
sasa katika nyanja ya elimu.
Rais Kikwete alitoa maagizo hayo jana katika
viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akitunuku hati Idhini kwa vyuo
vikuu na vyuo vishiriki nane vya hapa nchini baada ya kuwa vimekamilisha
taratibu zote za uanzishwaji wa chuo kikuu.
Alisema idadi ya wanafunzi wanaoingia katika
vyuo vikuu kwa sasa haitoshi kulinganisha na udahili wa wanafunzi katika vyuo
vingine vya nje.
kwa sasa idadi ya wanafunzi wanoingia vyuo vikuu
ni 78,735 kwa mwaka ambayo inapaswa kuongezwa hadi kufikia 80,000.
Alisema kwa sasa vyuo vikuu na vishiriki
vimeongezeka kutoka 37 awali hadi kufikia vyuo 52 kwa sasa.
Alifafanua kuwa
Serikali imedhamiria kuiinua sekta ya elimu nchini, kwa kuongezea bajeti ya
Wizara hiyo kutoka Sh. trilioni 2.1 kwa mwaka jana hadi kufikia Sh. trilioni
3.1 mwaka huu.
“Ongezeni idadi ya wakufunzi wenye sifa katika
vyuo, pamoja na kuwezeka zaidi katika mafunzo ya uzamivu na uzamili hata
mkiweza mkaazime wakufunzi nchi jirani,
” aisema Rais Kikwete.
Vyuo vilivyotunukiwa
hati Idhini ni Tumaini Makumira (Tuma), Mtakatifu Augustino cha Tanzania
(Saut), Kishiriki cha Ruaha (Ruco), Mount Meru (MMU), Arusha (UoA), Kishiriki
cha Tumaini Dar es Salaam (Tumadarco),Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela ya
Sayansi na Teknolojia Arusha (NM-AIST), Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia
Mbeya (Must).
Naye Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk.
Shukuru Kawambwa, alisema idadi ya wanafunzi wanaoingia vyuoni imeongezeka
kutoka 1,39,638 kwa mwaka 2010/11 hadi kufikia 1,66,484 kwa mwaka 2011/12 sawa
na asilimia 16.
Alisema katika kuboresha kiwango cha elimu, kuna
wahadhiri 44 waliopelekwa Ujerumani kuongeza ujuzi.
Mwakilishi wa Mkuu wa Chuo cha Saut, Titus Mdoe
alisema viongozi wa chuo wanatakiwa kuangalia mahitaji ya wanafunzi ili kuiinua
elimu nchini.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kirutheri
Tanzania, Dk. Alex Malasusa, alisema kutunukiwa kwa Idhini hiyo ni deni kubwa
kwa wamiliki wa vyuo nchini kuhakikisha kiwango cha elimu kinakua.
0 comments:
Post a Comment