BOMBA la gesi kutoka Mtwara
kwenda Dar es Salaam, linaanza kutandazwa leo likianzia mkoani Lindi. Kutokana
na hali hiyo, Serikali imeonya kwamba, yeyote atakayethubutu kuharibu
miundombinu ya bomba hilo, atachukuliwa hatua.
Taarifa hiyo ilitolewa juzi na Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, alipofanya ziara ya kukag
ua,
ubora wa vifaa, rasilimali watu na maandalizi ya miundombinu ya kutandaza bomba
hilo.
Wakati wa ziara hiyo ya siku moja, alikuwapo pia Balozi wa China nchini,
Lu Youging, viongozi mbalimbali wa Serikali na viongozi wa kampuni
zinazotandaza bomba hilo.
Profesa Muhongo alisema ameridhishwa na maandalizi
yanavyokwenda, kwa kuwa kuna vifaa vya kisasa na imara.
Kesho kutwa (leo), utandazaji
wa bomba unaanza rasmi na kwa maandalizi niliyoshuhudia, nina imani mradi huu
utakamilika kabla ya Desemba mwaka 2014.
“Naomba Watanzania wawe na imani
kubwa na watoe ushirikiano kwani utandazaji wa bomba utafanyika katika pande
zote mbili, kwa maana ya nchi kavu na baharini.
“Mradi huu ni wa gharama kubwa
na kama mnakumbuka, tulikopa fedha kutoka Benki ya Exim ambazo ni Dola za
Marekani bilioni 1.2 kwa masharti nafuu.
“Pamoja na kwamba nia yetu ni nzuri,
kuna baadhi ya watu wasiopenda maendeleo ya nchi hii, nataka kuwahakikishia
Watanzania wote, kwamba usalama wa miundombinu hii utakuwa shwari na kama mtu
anataka kushughulikiwa na Serikali, basi ajaribu kuihujumu atakiona cha mtema
kuni.
“Hapa tumeshuhudia Watanzania 45 walioanza kupata ajira kama madereva,
vibarua, kampuni za usafirishaji, huu ni mwanzo tu na ikifika sehemu ya
kuhitaji watu wenye utaalamu, wataajiriwa wenye utaalamu,” alisema Profesa
Muhongo.
Kwa mujibu wa Profesa Muhongo, mabomba yanayotandazwa ni ya aina
mbili yakiwamo ya inchi 36 na uzito wa tani tano na yenye inchi 24 yakiwa na
tani tatu ambayo alisema kwa ujumla wake yatadumu kwa miaka 30 na kama
yakitunzwa vizuri yatadumu hadi miaka 70.
“Tunataka ifikapo mwaka 2016, tuwe
na umeme wa megawati 3000 na mwingine wa ziada wa utakaokuwa ukiuzwa nje ya
nchi ikiwamo Kenya ambayo imeleta maombi ya kuuziwa megawati 1000,
” alisema.
Pamoja
na kufanya ziara hiyo juzi, Profesa Muhongo alisema itakuwa ni endelevu na
itakuwa ikihusisha waandishi wa habari.
Naye, Balozi Youging, alisema gesi ni
kitega uchumi kizuri ambacho kinaweza kuwaondoa Watanzania katika umasikini.
“China
ni moja ya nchi iliyonufaika na gesi na ndio maana raia wake ni wataalamu wa
nishati hiyo, naamini upatikanaji wa gesi hapa Tanzania, utasaidia Watanzania
kuondokana na matumizi ya mkaa na kuni.
Kwa upande wake, Meneja Mradi wa
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania, Mhandisi Baltazari Thomas, alisema
hadi sasa watu 163 wamepata ajira katika awamu ya kwanza na kati ya hao
Watanzania ni 68.
MTANZANIA
0 comments:
Post a Comment