Serikali ya Kenya kupitia wizara ya kilimo imetenga
shilingi milioni 500 kupiga jeki kilimo cha nazi katika mkoa wa pwani.
Waziri wa kilimo nchini Kenya Felix Koskei, anasema
serikali imejitolea kukuza zao hilo kwa sababu lina uwezo wa kuipa Kenya pato
la shilingi bilioni 25 kila mwaka.
Serikali ya Kenya imekuwa ikitoa shilingi milioni 80
kila mwaka kutumika kukuza zao hilo lakini waziri Koskei anasema ili kukuza zao
hilo ipasavyo inabidi fedha hizo kuongezwa.
Kwa sasa zao hilo linaipa Kenya mapato ya shilingi
bilioni 6.2 kila mwaka kutoka shilingi bilioni 3.2 miaka ya hapo awali.
Waziri huyo alisema serikali imepania kukuza sekta hiyo ya kilimo cha nazi kwa
asilimia 10 kila mwaka.
0 comments:
Post a Comment