Dkt.John Ashe, Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa
Joshua
Mmali Massoi.
katika kuelekea kuanza kwa mjadala wa wazi wa Baraza
Kuu la Umoja wa Mataifa hapo kesho Jumanne,leo baraza hilo limekuwa na kikao
cha ngazi ya juu kuhusu kufikia malengo ya maendeleo ya milenia na malengo
mengine ya kimataifa kuhusu watu wenye ulemavu.
Kikao hicho cha ngazi ya juu kikijumuisha washiriki
kutoka nchi mbali mbali ikiwemo watu wenye ulemavu kimejikita zaidi katika
azimio lenye lengo la kuweka maendeleo yanayojumuisha makundi yote hususan
kundi hilo muhimu katika ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015.
Rais wa mkutano wa 68 wa Baraza Kuu Dkt. John William
Ashe amesema azimio hilo lina vipengee muhimu vya kuhakikisha walemavu
hawaachwi nyuma iwapo jamii inataka kupata maendeleo endelevu.
“Jambo moja muhimu na la haraka ni kuhakikisha
majengo yote, vifaa na maeneo ya umma yanaundwa mahsusi kwa ajili ya kutumiwa
na kufikika kirahisi na watu wenye ulemavu na kuwa teknolojia mpya zinapatikana
ili kuboresha hali yao ya maisha na kuwapa uwezo wa kuendeleza shughuli zao za
kazi na kujumuika pamoja na jamii katika hali ya kawaida."
Mwanamziki mashuhuri wa Kimarekani, Stevie Wonder,
mwenye ulamavu wa macho, na ambaye pia ni balozi mwema wa amani wa Umoja wa
Mataifa, amezitaka serikali ziwekeze zaidi katika teknolojia ya kuwasaidia watu
wenye ulemavu.
"Ni lazima tuifanye teknoljia hii kupatikana
kwa watu wenye ulemavu kote duniani.
Ningependa
kuwaomba nyotte na nchi zote, hata kama ni kuwekeza fedha za serikali katika
teknolojia hii- ila sio tu ushuru upunguzwe, lakini pia kila mtu mwenye ulemavu aweze kujitegemea na
kujisikia huru."
Kwa upande wa mama huyu Gertrude Oforowa kutoka Ghana, amekuwa na
ujumbe huu kuhusu malengo ya maendeleo na watu wenye ulemavu.
"Ulemavu
ni lazima uwe sehemu ya maendeleo jumuishi, kama suala muhimu katika kila
uwanja, na malengo mahsusi, na njia ya kufuatilia uendelezaji na ujumuishaji
ili tuwe na ubora wa maendeleo kati ya sasa na 2015, na pia baada ya
2015."
0 comments:
Post a Comment