Bosi wa klabu
ya soka ya Barcelona Gerardo Martino, ameeleza kufurahishwa na kiwango cha
wanasoka wake kilichowapatia ushindi wa goli 4-1 dhidi ya Real Sociedad katika
mechi ya jana jumanne ya kuwania ubingwa wa ligi kuu ya soka ya nchini Uhispania
La Liga.
Ushindi huo wa nyumbani katika dimba la Camp Nou
umeendelea kuing'arisha Barca iliyopo kileleni ikiwa na alama 18 ifuatiwa na
Atletico de Madrid wakati nafasi ya tatu ikishikiliwa na Real Madrid.
Mabao ya awali yaliyopachikwa nyavuni na Neymar,
Lionel Messi na Sergio Busquets yaliiwezesha Barca kung'ara baada ya kutamatika
nusu ya kwanza ya kipindi cha mchezo huo.
Martino amesema atahakikisha wanatumia mbinu zaidi
kujakikisha wanaendelea kusalia nambari moja katika msimamo na tayari amebainisha
kuwa ataendelea na sera yake ya mzunguko na kuwapumzisha baadhi ya nyota wa
klabu hiyo.
Kwa hiyo Messi na Neymar hawatakuwapo katika mchuano
wa nusu fainali ili waweze kurejea hapo baadaye kabla katika fainali.
Matokeo mengine ya mechi za La Liga zilizotimua vimbi
hiyo jana ni ushindi wa Atletico de Madrid wa 2-1 dhidi ya Osasuna, Mlaga
waliibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Almera na Levante walitoka suluhu ya 1-1
dhidi ya Real Valladolid.
Mitanange inayotarajiw akushuhudiwa hii leo ni kati ya
Sevilla na Rayo Vallecano, Granada FC na Valencia wakati Real Madrid itakuwa na
kibarua dhidi ya Elche.
0 comments:
Post a Comment