Robert Boaz.
Wagonjwa waliokuwa wanasubiri kupata huduma na
watu wengine waliokuwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC ya mjini
Moshi, jana
walipata mshangao mkubwa baada ya uongozi wa hospitali hiyo kumnasa mtu
aliyejifanya daktari wa watoto akiwa kwenye chumba cha upasuaji.
Mtu huyo aliyefahamika kwa la, Alex Sumni Massawe (33), alikamatwa asubuhi ndani ya hospitali hiyo na
kuwekwa chini ya ulinzi mkali wa makachero wa Jeshi la Polisi waliokuwa
wamevalia nguo za kiraia, alikamatwa.
Inadaiwa kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa
amepanga kufanyia upasuaji wa ngozi, Makasi Tipesa ambaye anasumbuliwa na
ugonjwa huo baada ya kukutana na mama yake na kumuahidi kumpatia huduma kwa
malipo ya Sh. 200,000.
Habari zinasema kuwa kabla ya kukamatwa kwa Alex, mama mzazi
wa kijana huyo, mkazi wa Manispaa ya Moshi, Pamvelina Shirima, alikutana na
mtuhumiwa huyo katika baa moja maarufu mjini hapa iliyopo eneo la Dar Street
(jina limehifadhiwa) na kumtaka ampe kiasi hicho cha fedha kwa madai zitatumika
kuharakisha mwanaye wa kiume kufanyiwa vipimo vya upasuaji.
Ofisa Uhusiano wa
KCMC, Gabriel Chisseo, alisema kuwa daktari huyo aliwekewa mtego na uongozi wa
hospitali hiyo
baada ya baadhi ya wagonjwa kuripoti kutapeliwa na mtu ambaye
amekuwa akijitangaza kwamba ni daktari wa
“Huyu Alex Massawe tulimkamata asubuhi akiwa katika wodi ya upasuaji baada ya kupokea kiasi cha
Shilingi 200,000 kutoka kwa Pamvelina Shirima ambaye alimleta mwanaye afanyiwe
upasuaji wa ngozi.
Tunawataka wagonjwa wote kufuata taratibu ikiwamo
kutokubali kurubuniwa na watu ambao hawajavaa sare wala kuwa na vitambulisho
rasmi vya hospitali,” alisema Chisseo.
Alisema kijana huyo alikuwa
akihudhuria matibabu ya ngozi katika kliniki ya hospitalini hapo na kwamba
madaktari hawakuona umuhimu wa kumfanyia upasuaji.
Alisema mtuhumiwa huyo
alifanikiwa kupenya na kuingia wodini baada ya kutumia ujanja nje ya lango la
kuingilia akijifanya na yeye ni
mgonjwa.
Uongozi wa KCMC ulipoulizwa kufafanua
ilikuwaje mtuhumiwa huyo akaingia katika chumba cha upasuaji bila kuwa
mfanyakazi wa hapo, ulisisitiza kuwa aliingia kwa kupenya.
Chisseo alisema
mtuhumiwa huyo siyo mwajiriwa wao na kwamba baada ya kuhojiwa alidai kuwa
anafanya kazi katika hospitali hoja iliyoko Tabata, jijini Dar es Salaam.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz, alipotafutwa na NIPASHE kuzungumzia
tukio hilo, alithibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo ambaye anajitambulisha
kuwa ni daktari wa binadamu.
Kamanda Boaz alisema Jeshi la Polisi linaendelea
na uchunguzi wa tukio hilo na baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa
mahakamani.
Katika siku za karibuni yametokea matukio kadhaa ya baadhi ya watu
kukamatwa wakifanya kazi ambazo siyo taaluma zao.
Baadhi yao wamekamatwa
wakijiita maofisa usalama wa Taifa, polisi na askari wa usalama barabarani.
0 comments:
Post a Comment