Dk John Magufuli.
Serikali imetakiwa kuajiri wahandisi wa
nchini na kuacha tabia ya kuajiri watu kutoka nje ya nchi.
Kauli hiyo imetolewa na
Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli, jijini Dar es Salaam katika mkutano wa
mwaka wa wahandisi.
“Mapinduzi katika nchi zilizoendelea yasingekuwapo bila ya
kuwapo kwa fani ya uandisi, hivyo ni vyema serikali ikawapa kipaumbele
wahandisi wazawa kwani wana vigezo na viwango vilivyopitishwa na bodi,”
alisema Dk. Magufuli.
Dk. Magufuli aliongeza kuwa “tusipokua
makini na kufumbia macho kama suala la gesi tutaishia kuwa wasindikizaji tu ,”
Pia
alisema kwamba serikali jumla ya imetenga Sh. milioni 500, katika mwaka wa
bajeti 2013/14 kwa ajili ya kusaidia mafunzo ya wanafunzi wa fani hiyo.
Vilevile,
aliwaasa wahandisi wote kuwa waangalifu, wajitume kwa bidii na kuacha tabia
ya kuoneana wivu katika kazi na kuwa na desturi kwa kushindana
kibiashara na kwa ushirikiano.
Aliwataka wafanye kazi kwa weledi na
wajali kazi kwanza na kwa maslahi ya Taifa, kujali viwango na
kuepukana na tabia ya kupokea rushwa.
Mwenyekiti wa Bodi ya
Wahandisi, Profesa Ninatubu Lema, alisema fani hiyo inakabiliana na
changamoto za utekelezaji wa miradi ya kiuhandisi.
Pia alisema, bodi hiyo
imepewa mamlaka ya kusajili wahandisi na kampuni zote za kihandisi na kuwapa
leseni na masharti yake.
0 comments:
Post a Comment