Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi
katika uzinduzi wa kongamano maalum kuhusu shughuli za uwekezaji kwenye Ukanda
wa Magharibi unaojulikana kama Ukanda wa Ziwa Tanganyika.
Mkuu wa Mkoa wa
Kigoma, Issa Machibya, alisema jana jijini Dar es kuwa, kongamano hilo
litafanyika mwezi ujao katika Halmashauri ya Wilaya ya Ujiji mkoani Kigoma na
Rais Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.
Kongamano hilo litahudhuriwa na
washiriki kutoka ndani na nje ya nchi, yakiwamo mabaraza ya biashara nchini.
Kongamano
kama hilo ni la tatu kufanyika katika ukanda huo unaojumlisha mikoa ya Kigoma,
Rukwa na Katavi, huku mawili ya mwanzo yakiwa yamefanyika katika Halmashauri ya
Wilaya ya Mpanda.
0 comments:
Post a Comment