Rais Jakaya
Kikwete akiwa katika mazungumzo na marais; Paul Kagame (kushoto) wa Rwanda,
Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini na Rais Yoweri Museveni (wa pili kulia) wa
Uganda wakati wa mkutano wa wakuu wa nchi za Maziwa Mkuu.
Rais Jakaya Kikwete amekutana kwa faragha na Rais
wa Rwanda, Paul Kagame katika mazungumzo yanayoelezwa kuwa yalikwenda vizuri.
Taarifa
ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais iliyotolewa jijini Dar es Salaam jana
ilisema kuwa mazungumzo hayo yaliyodumu kwa zaidi ya saa moja, yaliwaridhisha
viongozi hao.
“Viongozi hao wamekutana kwa zaidi kidogo ya saa moja katika
mkutano uliofanyika kwenye Hoteli ya Munyonyo Commonwealth Resort, nje kidogo
ya mji wa Kampala, Uganda, “ ilisema taarifa ya Ikulu.
Taarifa hiyo iliongeza
kuwa katika mazungumzo hayo, Rais Kikwete na Rais Kagame wamekubaliana
kuendelea kushirikiana katika kujenga uhusiano mzuri na wa kihistoria uliopo
kati ya nchi hizo mbili.
Kikwete na Kagame wapo Uganda kuhudhuria Mkutano wa
Nchi Wanachama wa Umoja wa Kimataifa wa Maziwa Makuu – “International
Conference on the Great Lakes Region (ICGLR)” uliofanyika jana katika Hoteli ya
Munyonyo Commonwealth Resort.
Viongozi wengine ambao walihudhuria Mkutano huo
ni pamoja na Rais Yoweri Museveni wa Uganda ambaye ni Mwenyekiti wa ICGLR na
mwenyeji wa Mkutano huo, Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini, Rais Joseph Kabila wa
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa
Afrika (AU).
Rais Kikwete na ujumbe wake aliwasili Kampala jana asubuhi
akitokea mjini Dodoma ambako aliwaapisha Makatibu Wakuu watatu na Naibu
Makatibu Wakuu wawili iliyofanyika Ikulu Ndogo, Dodoma.
Hata hivyo, taarifa
ya Ikulu haikufafanua zaidi kama mazungumzo hayo yaligusa nini mahususi hasa
juu ya ushauri wa Rais Kikwete juu ya Rwanda kuzungumza na waasi, na hali ya
mapigano ndani ya DRC yanayoendelea sasa ambayo waasi wa M23 wanaodaiwa
kusaidiwa na Rwanda wamefurahishwa na vikosi vya Kulinda Amani vya Umoja wa
Mataifa vinavyoongozwa na wanajeshi wa Tanzania.
Tangu Rais Kikwete ampe
ushauri Rais Kagame kuwa afanye mazungumzo na waasi wa nchi hiyo waliokimbilia
DRC kumekuwa na hali ya kuzorota kwa uhusiano kati ya Rwanda na Tanzania.
Ushauri
wa Rais Kikwete umekuwa ukilaumiwa na baadhi ya viongozi wa Rwanda na hata
kufikia vyombo vya habari vya nchi hiyo kumtusi.
0 comments:
Post a Comment