JASON NYAKUNDI.
Tarehe Kumi na Tano Septemba ni siku ya demokrasia
duniani. Mwaka huu ujumbe ni kuimarisha sauti za demokrasia.
Umoja wa Mataifa unasema kuwa lengo la ujumbe huu ni
kuangazia mwanga umuhimu wa sauti za wananchi kupitia wao wenyewe na hata
wawakilishi wao katika masuala ya kisiasa, kijamii na kiuchumi.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon katika
ujumbe wake wa siku hiyo anatoa wito kwa viongozi duniani, kusikiliza,
kuheshimu na kuchukua hatua muafaka kwa sauti za wananchi iwe zinatoka moja kwa
moja kwa wananchi wenyewe au kupitia wawakilishi wao.
Je wigo wa demokrasia uko vipi katika hali ya kawaida?
Sauti zinasikilizwa? Viongozi wanawakilisha wananchi?Hilo ni swali tu Tafakari.
0 comments:
Post a Comment