DIWANI ATHUMANI
“PRESS RELEASE” TAREHE 14. 09. 2013.
WILAYA YA RUNGWE –
MHE. DIWANI KATA YA KIWIRA AKAMATWA KWA
TUHUMA ZA KUFANYA MAPENZI NA MWANAFUNZI.
TUHUMA ZA KUFANYA MAPENZI NA MWANAFUNZI.
|
§ MNAMO TAREHE
12.09.2013 MAJIRA YA SAA 19:30HRS HUKO KATIKA KITONGOJI CHA
KIBUMBE KATA YA KIWIRA – TUKUYU WILAYA YA
RUNGWE MKOA WA MBEYA, RAPHAEL S/O FRANK, MIAKA 42, KYUSA, MKULIMA
NA MKE WAKE SUZANA W/O FRANK, MIAKA 38, KYUSA, MKULIMA WOTE WAKAZI WA
KIBUMBE KIWIRA – TUKUYU WAKIWA NYUMBANI KWAO WALIGUNDUA KUTOWEKA KATIKA
MAZINGIRA YA KUTATANISHA KWA MTOTO WAO AGNES D/O RAPHAEL, MIAKA 18,
KYUSA, MWANAFUNZI KIDATO CHA NNE SHULE YA SEKONDARI KIWIRA HIVYO JITIHADA
ZA KUMTAFUTA ZILIANZA MARA MOJA USIKU KUCHA BILA MAFANIKIO.
§ MNAMO TAREHE
13.09.2013 MAJIRA YA SAA 06:00HRS WAZAZI HAO BAADA YA KUONA MTOTO
WAO HAKULALA NDANI KAMA ILIVYO KAWAIDA WALIAMUA KWENDA KATIKA KITUO CHA POLISI
KIWIRA NA KUTOA TAARIFA YA KUPOTELEWA NA MTOTO. HATA HIVYO
MAJIRA YA SAA 09:00HRS MTOTO WAO AGNES D/O RAPHAEL ALIRUDI NYUMBANI NA
WAZAZI WAKE WALIPOMHOJI JUU YA MAHALI ALIPOKUWA ALIWAJIBU KUWA
ALIKUWA NA MHE DIWANI WA KATA YA KIWIRA [CHADEMA]
LAURENT S/O MWAKALIBULE, MIAKA 28, KYUSA, MKAZI WA KIWIRA – KATI NA
KWAMBA WALILALA KATIKA NYUMBA YA MDOGO WAKE NA DIWANI HUYO AMBAYE JINA
LAKE BADO KUFAHAMIKA NA KUWA KABLA YA KUKUTANA WALIWASILIANA KWA NJIA
YA SIMU YA KIGANJANI.
§ MTUHUMIWA AMEKAMATWA,
UPELELEZI WA SHAURI HILI UNAENDELEA .
§ KAMANDA WA POLISI MKOA
WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA
JAMII HASA WANAFUNZI KUJIEPUSHA NA MADHARA YA KUFANYA MAPENZI
[NGONO] KWANI NI HATARI KWA AFYA ZAO NA PIA KWA MAISHA YAO YA
BAADAE BADALA YAKE WAZINGATIE ZAIDI MASOMO KWA FAIDA YAO , VIZAZI VYAO NA
TAIFA KWA UJUMLA..
[DIWANI ATHUMANI -
ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Post a Comment