Uthubutu na nia njema
yenye uzalendo ndani yake ndivyo vilivyowafanya watu 18 washiriki katika
matembezi ya kupinga ujangili nchini "Walk for Elephants"..
Matembezi haya yalipewa jina la “Walk for Elephants” na yamedumu
kwa muda wa siku 19 kabla ya kupokelewa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,
Lazaro Nyarandu Alhamisi ya Septemba 12 mwaka 2013.
Nyarandu ameunga mkono
uzalendo huo kwa vitendo pale alipotembea kwa mguu kutoka Ubungo hadi Mnazi
Mmoja, akatumia zaidi ya saa moja na nusu akiambatana na Mwenyekiti wa Kamati
ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli na Mkurugenzi wa idara
ya wanyama pori, Profesa Alexander Songorwa pamoja na Mkurugenzi wa African
Wildlife Trust, Pratik Patel.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyarandu
(katikati), akiwa na wadau wa vita dhidi ya ujangili, Kulia kwake ni Meneja wa
maendeleo ya jamii kutoka Friedrikin Group of Comanies, Aurelia Mtui, upande wa
kushoto wa Nyarandu ni Faraja Nyarandu na Nancy Sumari pamoja na askari wanyama
pori kutoka Arusha.
Nyarandu akaweka
bayana kuwa matembezi hayo ya kupiga vita ujangili nchini yamefanyika wakati
ambapo kuna ongezeko kubwa la ujangili, nchini hususan ujangili wa tembo.
Ujangili ambao
unasababishwa na mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa bei ya meno ya
tembo katika masoko haramu huko Mashariki ya Kati na Asia na Kuimarika na
kuongezeka kwa magenge ya ujangili (poaching syndicates) pamoja na ubora wa
mawasiliano.
Sababu nyingine ni
Kudorora kwa uchumi na kuongezeka kwa umasikini katika jamii, hivyo kufanya
watu wengi kujiingiza kwenye ujangili cha uhalifu mwingine, Uroho wa kutaka
utajiri wa haraka haraka ambao umewafanya baadhi ya wafanyabiashara wakubwa na
wadogo na watumishi wa umma kujiingiza katika ujangili na Rushwa na mmomonyoko
wa maadili katika jamii kwa jumla.
Naibu Waziri, Lazaro Nyarandu akipokea hundi ya dola za
kimarekani milioni 250 kutoka kwa Mkurugenzi
wa Friedrikin Conservation Fund, Mitchel Allard kwaajili ya
kutekeleza shuguhuli za vita dhidi ya ujangili.
Mkurugenzi wa Friedrikin Conservation Fund,
Mitchel Allard.
Ujangili umeelezwa kuchangia
sana katika kupungua idadi ya tembo nchini kutoka 350,000 miaka ya 1960 hadi
110,000 mwaka 2009. Idadi ya tembo wanaouawa na majangili inazidi
kuongezeka kila mwaka
Matembezi hayo
yameandaliwa na shirika la African Wildlife Trust yamehitimishwa leo mmnazi
mmoja ambapo wadau mbalimbai na wananchi walifika kuwaona mashujaa waliotembea
katika safari hiyo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyarandu
(anayeongea na simu) akiongoza matembezi ya kupinga ujangili kuelekea mnazi
mmoja baada ya kuyapokea Ubungo, kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge
ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli na wadau wengine katika
mapambano ya ujangili
0 comments:
Post a Comment