Mwanamke raia wa Uingereza,
Samantha Lewthwaite aka The White Widow, *anahisiwa* kuongoza kundi la magaidi
wa Al-Shabaab walioivamia mall maarufu ya Westgate ya jijini Nairobi nchini
Kenya jana na kuwaua watu zaidi ya 68 na kujeruhi wengine zaidi ya 175.
Tayari mashirika makubwa ya habari duniani yakiwemo, CNN, The Sun na IBTimes
yameandika habari kuhusu uwezekano wa mwanamke huyo kuwa kiongozi wa magaidi
hao walioshambulia Westgate.
Nayo akaunti ya Twitter ya
American Jihad Watch @watcherone, imepost picha ya gaidi wa kike iliyedai
ilipigwa na camera za ndani ya mall huyo na kudai kuwa ‘huenda’ akawa ni The
White Widow. “Female jihadi caught on mall camera at Westgate Centre Shopping
mall earlier yesterday may be infamous ‘White Widow’, imesomeka tweet hiyo.
Kwa mujibu wa baadhi ya watu
waliokolewa kwenye mall hiyo, miongoni mwa magaidi hao alikuwepo mwanamke wa
kizungu.
Kwa mujibu wa CNN, magaidi watatu ni wa Marekani, mmoja wa Kenya, Uingereza, Finland na wawili wa Somalia. Bado wamo ndani ya mall hiyo.
Hata hivyo Kwa mujibu wa mtandao wa Telegraph, jana usiku ofisa wa shirika la
kupambana na ugaidi Kenya alikanusha taarifa kuwa Samantha Lewthwaite anaweza
kuhusika na shambulio la jana.
Samantha Lewthwaite aka The White Widow ni nani?
Ni mwanamke anayetafutwa kwa udi na uvumba kwa kuhusika kwake kwenye matukio
mbalimbali ya kigaidi nchini Uingereza na Afrika Mashariki. Yeye ndiye
aliyepanga shambulio la kigaidi jijini London la mwaka 2005 lililosababisha
vifo vya watu 52 ambapo mume wake Jermaine Lindsay alijitoa muhanga.
Akitokea Aylesbury, Buckinghamshire, nchini Uingereza, The White Widow kwa sasa ni kiongozi wa juu wa mashambulio ya Al Shabaab nchini Kenya na Somalia. Mwanamke huyo anadaiwa kuwa mfadhili mkuu wa shughuli za kundi hilo la kigaidi.
Mwezi May hati ya kumkamata ilitolewa baada ya kushindwa kufika mahakamani
nchini Kenya kwa kesi ya kutengeneza bomu.
0 comments:
Post a Comment