Waziri wa
mambo ya ndani wa Kenya Joseph Ole Lenku amesema Idadi kubwa ya mateka
wameokolewa na Jeshi la Kenya baada ya kudhibiti sehemu kubwa ya jengo la
kibiashara Westgate katika operesheni ya kuhakikisha wanawakomboa mateka
waliokuwa wakishikiliwa na wanamgambo wa kundi la Alshabab ambao walivamia na
kuteka eneo hilo jumamosi mchana.
Ole Lenku ameongeza kuwa mpaka sasa Idadi rasmi ya
watu waliopoteza maisha imefikia 62 wakati majeruhi wakifikia 175 wakati
wapiganaji wawili wa Alshabab wamethibitika kuuawa na wengine baadhi
kujeruhiwa.
Misaada ya aina mbalimbali imeendelea kutolewa ikiwemo
zoezi la uchangiaji damu kwa ajili ya kuokoa maisha ya majeruhi ambao wengine
wamefanyiwa upasuaji.
Tukio la mashambulizi yaliyofanywa na wanamgambo wa
Al-Shabab kwenye maduka ya westgate nchini kenya limezusha hofu miongoni mwa
mataifa ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na nchi za Maziwa
makuu.
Serikali za Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi
zimelaani shambulio hili na kutoa pole kwa rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja
na wananchi wa taifa hilo ambao wamepoteza ndugu zao.
Wachambuzi wa mambo wanasema kuwa kenya kwasasa
inakabiliwa na changamoto kubwa ya kiusalama hali ambayo ni lazima nchi jirani
ziimarishe usalama kwenye mipaka yao.
0 comments:
Post a Comment