Klabu ya Real
Madrid ya huko Uhispania imeilaza klabu ya Getafe kwa mabao 4 – 1 ikiwa ni
michuano ya ligi kuu nchini humo.
Timu hiyo ilianza vibaya mchezo huo kwanza
mchezaji Gareth bales alijeruhiwa wakati akifanya mazoezi ya kupasha mwili moto
kabla ya kuanza kwa mchezo, na katika dakika tano za mchezo mshambuliaji Angel
Lafita aliliona lango la Real na kuandika bao la kwanza.
Real Madrid wakiwa nyumbani walitakiwa kuonyesha uwezo
na kusawasizisha katika dakika ya 19 na mchezaji Pepe, huku Christiano Ronaldo
akipachika mawili na kuandikisha bao la 208 na 209 katika klabu hiyo na
kumshinda Hugo Sanchez ambaye anachukuwa nafasi ya tano katika wafungaji wa
mabao mengi katika klabu hiyo.
Mshambuliaji Isco ndiye aliye pachika bao la 4 la Real
Madrid na kuwafanya mashabiki wa klabu hiyo kulala roho baridi.
Katika matukio mengine FC Betis Séville ilitoka sare
ya bila kufungana na Granada FC. Valence ikaitandika FC Seville mabao matatu
kwa moja, huku Celta Vigo na Cillarreal zikashindwa kufungana na kulazimishana
sare ya 0-0.
0 comments:
Post a Comment