Timu ya taifa
ya kikapu nchini Ufaransa, imetwaa Kombe la mpira wa kikapo katika mashindano
ya Ulaya ikiwa ni mara ya kwanza katika Historia ya mchezo huo.
Vijana wa Les Blues waliishinda Litunia kwa vikapo 80
kwa 66 ikiwa ni tofauti ya vikapo 14, ambapo wataalamu wa mchezo huu wanasema
ni tafauti kubwa.
Wachezaji nyota waliotamba katika mchezo huo ni pamoja
na Boris Diaw, Nicolas Batum pamoja na Tony Parker alieteuliwa kuwa mchezaji
bora wa michuano hiyo ya mpira wa kikapo barani Ulaya.
Kulikuwepo na shaka upande wa Timu hiyo ya Ufransa,
kwani walianza vibaya kwa kushindwa mara tatu katika mechi nane.
Lakini baadae vijana hao wa le Blues wamekamilisha
kuwa washindi wa michuano hiyo pale walipoanza kuinyuka Slovenia wenyeji
wa michuano hiyo mbele ya mashabiki wake na baadae Uhispania bingwa mtetezi wa
kombe hilo.
0 comments:
Post a Comment