Imeelezwa kuwa Tanzania inaweza kuzalisha mamilionea 100 kila mwaka iwapo
vijana wenye mawazo bora ya ujasiriamali watawezeshwa kuwekeza katika raslimali
za taifa.
Mwenyekiti mtendaji wa IPP Dk Reginald Mengi ameyasema hayo
jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya kuwazawadia washindi wa mwezi augosti
wa shindano aliloliasisi la kutwiti wazo bora la kuondoa umaskini nchini.
Mratibu wa shindano hilo ambaye pia ni mkurugenzi mkuu wa
taasisi ya uongozi na ujasiriamali (IMED), Dr Donath Olomi amesema jumla
ya twiti 979 zilishindwanishwa na kumtaja mshindi wa kwanza, aliyejinyakulia
zawadi ya shilingi milioni moja kuwa ni Bi Lilian Wilson ambaye ni mwanafunzi
wa chuo kikuu cha ardhi jijini Dar es salaam.
Aidha amemtaja mshindi wa pili aliyezawadiwa shilingi laki
tano kuwa ni Bi Susana Senga ambaye ni Msanifu kurasa wa gazeti la
Jamhuri, na nafasi ya tatu, iliyoambatana na zawadi ya shilingi laki tatu
ilikwenda kwa Bw. Ombeni Kaaya mkazi wa Nzega anayefanya biashara
ya mgahawa na saloon ya kike.
ITV.
0 comments:
Post a Comment