Mawakili wa utetezi dhidi ya maombi ya
Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ya kukata rufaa dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa
Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Dar es Salaam, Abdallah Zombe, na wenzake
wanane nje ya muda, wameomba mahakama kutupilia mbali maombi hayo kwa sababu
hayana mashiko ya kisheria.
Madai hayo yalitolewa jana kwa nyakati tofauti na
mawakili hao; Richard Rweyongeza, Majura Magafu na Denis Msafiri wakati
wakijibu hoja za Jamhuri mbele ya Jaji Aloyisius Mujuluzi aliyepangiwa
kusikiliza maombi hayo.
Kabla ya kuwasilisha pingamizi hilo, upande wa Jamhuri
ukiongozwa na Mawakili wa Serikali Waandamizi, Edward Kakolaki na Timon Vitals,
waliomba mahakama hiyo kukubali kuyasikiliza maombi yao kwamba kwa kufanya hivyo
hakuna upande utakaopata madhara.
Kakolaki alidai kesi hiyo ina maslahi ya
taifa na kwamba jamii inasubiri kujua nini hatma ya maofisa hao wa jeshi la
polisi dhidi ya tuhuma zilizokuwa zinawakabili.
Jaji Mjuluzi alisema baada ya
kusikiliza hoja za pande zote mbili atatoa uamuzi Oktoba 17, mwaka huu.
Zombe
na wenzake walikuwa wakikabiliwa na kesi ya mauaji ya wafanyabiashara watatu wa
madini wa Morogoro na dereva teksi.
Mbali na Zombe, wajibu rufani wengine ni,
Christopher Bageni, Ahmed Makele, Jane Andrew, Emmanuel Mabula, Michael Shonza,
Abeneth Saro, Rajabu Bakari na Festus Gwabisab.
0 comments:
Post a Comment