2.
Ile sauti mnayosikiaga ikisema TONGWE RECORDS BEIB siyo ya ROMA ni
JOSLIN!!ambae naye ni miongoni mwa wasanii walio chini ya tongwe!! plus
KAMIKAZE/JOS MTAMBO/DOMO KAYA/SAIGON/NORMAN WA BSS/
3.
Kuna J. MURDER ambae ndiye CEO wa tongwe records, na kuna J.RYDER ambaye ndiye
anagonga midundo ya TONGWE RECORDS. watu wawili tofauti!!
4.
Tongwe records ni studio zilizopo daresalaam mitaa ya masaki/ dakika kama 3 tu
kutokea coco beach!! na haipo kigamboni kama wengi wanavyodhani!! lakini tanga
kuna kijiji kinaitwa TONGWE na ndicho kijiji ama himaya ya J. MURDER!! ambaye
ndiye huyo mmiliki!!
5.
Sijawahi kufungwa wala kwenda jela/ sijawahi kuitwa ikulu/ nyimbo zangu za
awali tanzania/ mr president ndiyo zilipigwa stop kupigwa ktk baadhi ya vituo
vya radio, kwa sababu zao binafsi!!
6.
Mimi kwetu ni TANGA nimezaliwa na kukulia na kusoma na kuanza muziki TANGA/
kiasili ni mpare(SAME KILIMANJARO) na mama ni mchaga!! kikabila utani
unaruhusiwa, mpare mtani wake mchaga, ndiyo maana mchaga siku zote namuona ni
mtani wangu(MSIPANIKI)!! nadumisha mila ya utani!!
7.
Katika face book account yangu niitumiayo ni hii ya Roma Tongwe na pia kuna
page yangu inaitwa R.O.M.A na kuna group inaitwa ONGEA NA ROMA baaaasiii!!
lakini kuna wana tu kwa mapenzi yao ama kwa uduanzi wao huamua na wamefungua
akaunti kibao wakijiita Roma mkatoliki/Roma mtanzania/Roma Tanga/ na zingine,
tena ukizipitia jamaa wana marafiki wengi kuliko hata mimi, na wanazi-run kama
mimi yaani nao wanapost kabisa ETI OYAA MOROGORO HERE I COME…hahahahahha bongo
bana!!
8.
Aliyeimba chorus ya 2030 ni mtoto wa rafiki yangu anaitwa STORY, ni mtoto wa
miaka 7hiviii!! lakini chorus ile iliimbwa miaka ya 90 naa zamani sana na binti
mmoja ambaye kwa sasa amekuwa sana!!!
9.
Nilianzisha mtindo wakuuza nyimbo zangu on-line(BUT LOKO) na kama trial
nilianza na 2030(tsh 3000/=), ilikuwa ni nyimbo inayohitajika sana na wenye
mapenzi na kuujua umuhimu wa kazi ya sanaa walinunua(sio woote) ila kati ya
marafiki 5000 wa fb walinunua takribani watu 500 tu!! hadi sasa siwezi na
sijawahi mtumia mtu nyimbo yangu akiniomba for free!! it z for sale!! 3000 per
track!! otherws tumia indirect ways!!
10.
Natoa ngoma 1 kwa mwaka!! tokea naanza game hii, ndiyo utaratibu niliojiwekea,
najaribu kufanya LIVING SONGS!!(nyimbo zinazodumu/zinazoishi, kana kwamba
ukisikia jogoo la tanzania linawika sasa uamke kwenye kiti chako turuke ruke!!)
wapo artist ambao ndani ya miezi 6 wanatoa ngoma hata 4, na zinaweza feli zote,
ama zikafaulu zote!! ni sawa kwa upande wao!!ndio njia waliyoichagua!! So toka
tanzania 2008 hadi 2030 iliyotoka december 29 2012 siku moja kabla ya 2013!!
ipo hivo!!
kwahiyo nadaiwa ngoma mpya mwaka huu!! na SOON ZITATOKA VIDEO 2 ZA ROMA!!
kwahiyo nadaiwa ngoma mpya mwaka huu!! na SOON ZITATOKA VIDEO 2 ZA ROMA!!
0 comments:
Post a Comment