Nchi za Afrika mashariki na kati ikiwa, Tanzania, Burundi, na Rwanda zimetiliana saini
makubaliano ya pamoja ya mradi wa kuzalisha umeme wa Rusumo Falls.
Mradi huo utagharimu dola za kimarekani milioni 340 na
unatarajiwa kuinua kiwango cha umeme na pia uzalishaji viwandani pindi tu
utakapokamilika.
Waziri wa kawi nchini Burundi Manilakiza Cone anasema
mradi huo unatarajiwa kuipa nchi yake megawati muhimu za umeme kuweza kuendeleza shughuli za uzalishaji viwandani.
Waziri wa kawi nchini Tanzania Sospeter Muhongo
anasema kuanza kwa mradi huo ni jambo la kutia moyo kwa nchi yake kwani mradi
huo umekuwa ukikusudiwa tangu mwaka wa 1974.
Mradi huo unatarajiwa kutoa mega wati 80 za umeme.
0 comments:
Post a Comment