Msemaji wa hospitali ya huko amesema, waliouawa ni
pamoja na askari wawili, watoto 7, na wanawake 34, na idadi ya vifo huenda
ikaongezeka kwa kuwa baadhi ya majeruhi wako mahututi.
Baada ya mashambulizi hayo kutokea, waumini wengi
wakristo walifanya maandamano katika miji mbalimbali nchini Pakistan, wakiitaka
serikali ihakikishe usalama wa makanisa nchini humo.
Rais Mamnoon Hussein wa Pakistan na waziri mkuu Bw.
Nawaz Sharif walilaani vikali mashambulizi hayo.
Habari nyingine zinasema kundi la Taliban nchini
Pakistan limetangaza kuwajibika na mashambulizi hayo, na kusema wataendelea
kuwashambulia watu wasio waumini wa dini ya kiislamu, hadi ndege za Marekani
zisizo na marubani zitakaposimamisha mashambulizi katika sehemu ya kaskazini
magharibi mwa Pakistan.
0 comments:
Post a Comment