Bila
shaka umewahi kusikia ule wimbo wa njiwa peleka salamu! hahaha njiwa
wanaaminika kutumiwa kupeleka ujumbe wa siri katika mambo mengi lakini mara hii
ni ndege aina ya Mumbi (Swan) amekamatwa na kuwek
wa chini ya ulinzi huko Misri akidaiwa kuwa mpelelezi aliyetumwa na
wafaransa
Mapema wiki hii ndege Mumbi
alikutwa nyuma ya jengo la gereza huko Qena akiwa amejikunyata huku mwilini
mwake akiwa amefungwa kifaa cha elektroniki kilichodhaniwa kuwa ni cha upelelezi.
Mkazi mmoja wa eneo hilo baada ya kumwona ndege huyo alimchukua na kumpeleka
kwenye mamlaka ambako polisi walimuweka kizuizini (lupango).
Baada ya uchunguzi wa awali Mkuu wa mambo ya
usalama wa Qena Ayman Abdallah alisema kifaa kilichofungwa kwa ndege huyo ni
cha kufuatilia mwenendo na uhamaji wa ndege kinachotumiwa na wanasayansi wa
Ufaransa na kuahidi kumwachia ndege huyo baada ya uchunguzi kumalizika.
Gazeti la serikali limempongeza
mtu aliyehusika kumkamata ndege huyo kwa kuonyesha uzalendo wake na umakini
katika kulinda maslahi ya taifa huku ndege huyo akiendelea kubaki korokoroni
hadi hapo mamlaka zitakapokamilisha uchunguzi wote na kumwachilia huru.
Si mara ya kwanza kutokea matukio
ya wanyama na ndege kudhaniwa kuwa ni wapelelezi hasa wakati wa vita na wakati
mgumu kama wanaoupita Misri sasa.
Chanzo: NYDailyNews and abcLocal
0 comments:
Post a Comment